• Sat. Sep 14th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wanandoa Wahimizwa Kutatua Matatizo kwa Njia ya Amani

Jun 21, 2021
479 300

Wanandoa katika eneo la Homabay wameombwa kusuluhisha migogoro yao kwa njia inayostahili kama vile kuwashirikisha wazee wa jamii na viongozi wa kidini.

Hii ni baada ya Afisa mmoja wa askari katika kijiji cha Kabuor, kaunti ndogoya Rachuonyo kumjeruhi mke wake kwa kucha sehemu zake za siri.

Kulingana na familia ya Mwanamke aliyejeruhiwa, jamaa huyo ambaye ni askari alireje nyumbani kutoka kazini na kuuchukuwa simu ya mkewe na kuanza kuangalia wale aliokuwa amezungumza nao. Hapo ndipo alifikiri mkewe alikuwa na mpango wa kando na naibu wa mwalimu mkuu wa shue ya msingi iliyo karibu nao.

“uchunguzi huu ndio ulimfanya awe na Hasira na na kumuuliza msichana Wangu ni kwa nini alikuwa ameongea na mwalimu yule mara nyingi,” alisema Alfeus Ong’oy baba ya Mwathiriwa.

Alisema kuwa juhudi zake za kumweleza kuwa walikuwa wakizungumza kuhusu maswala ya elimu ya wanao watatu wanaosoma shuleni humo hazikufua dafu na hapo ndipomumewe alipoanza kumpiga na kumdunga kwa kucha sehemu za siri.

“Nina wasiwasi kwa kuwa mwanangu amejeruhiwa vibaya. Kama anaweza kumtendea unyama huu basi hata anaweza kumuuwa,” aliongeza Ong’ou.

Mwathiriwa aliripoti Tukio hilo katika kituo cha polisi cha Oyugis na uchunguzi umeanzishwa ilikumnasa kumshukiwa huku Mwanamke huyo akiepata matibabu katika hospitali ya Rachuonyo Kusini. Akidhibitisha Tukio hilo, naibu Kamishna wa Rachuonyo David Kiprop, amekashifu kitendo hicho na kusema sio ubinadamu katu.

“mbona umjeruri mkeo hata kama ameenda kinyume na ndoa yenu?” aliuliza Kiprop.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *