• Thu. Sep 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Uchunguzi: Magari ya PSV Yapuuza Masharti ya Kupambana na Corona

Jun 21, 2021
398 300

Magari mengi ya uchukuzi wa umma yanaonekana kurejelea mtindo wa kubeba abiria wengi kupita kiasi.

Hii ni licha ya serikali kupitia wizara ya Afya kuweka masharti kwa magari hayo kubeba idadi nusu ya abiria.

Abiria katika gari la Kampuni ya Likana jumapili hii walimfokea dereva na kondakta wake baada yao kujaza gari kupindukia.

“Tulipokua tunaingia katika gari hili, mlisema kuwa mnafuata masharti ya a wizara ya afya. Mbona sasa mnabeba kupita kiasi?”walifoka abiria waliokuwa na gadhabu.


“Kwanza ‘huyu’, hajalipia, mbona awe kondakta na gari linapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa?” Waliongeza kwa gadhabu.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Taarifa News matatu nyingi hazifuati Sheria hizi huku msambao wa virusi vya Korona ikizidi.

Tulipozungumza na dereva alisema kuwa hali ya uchumi ndio inayosababisha masharti haya kukiukwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *