Miili ya watoto wawili chini ya miaka kumi walioripotiwa kupotea katika eneo la Buruburu, Juni 30 na Julai 1 wamepatikana wakiwa wamefariki.
Miili ya Mvulana na msichana hao ilipatikana Jana, Julai 13 ikiwa imetupwa katika eneo la Spring Valley, Westlands.
Mshukiwa Mkuu katika utekaji nyara huo alikamatwa.
Maafisa wa Polisi walieleza Taarifa News kuwa walimnasa mshukiwa huyo akiwa katika nyumba yake ya kukodi, Kitengela Kaunti ya Kajiado na akawapeleka katika eneo hilo ambako walipata miili hiyo.
“Uchunguzi umebaini kuwa watoto hawa waliuawa baada ya kutekwa nyara Buruburu kutokana na kutoelewana na waliokuwa wamepanga njama hiyo,”alisema afisa wa Upelelezi katika kituo Cha Polisi Cha Gigiri.
Maafisa wa Polisi wa Spring Valley walipeleka miili hiyo katika Makafani itakapofanyiwa upasuaji.