Chama cha wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Nairobi,sasa kimetishia kufanya maandamano kali ikiwa serikali ya kaimu gavana wa Nairobi Ann Kananu itaweka wafanyikazi wa kaunti ndani ya bima ya serikali ya NHIF.
Kulingana na muungano huo NHIF haitawapa hudumu kama walivyokuwa wakipata kutoka kwa bima binafsi kama vile AAR na hivyo basi hawatakubali hilo kufanyika.
Benson Oliang’a akizungumza na Taarifa News ameweka wazi hawatakubali kuingia chini ya bima hiyo.
‘‘Hakuna asiyejua shida ya NHIF na hivyo basi sisi kama wafanyikazi hatutakaa chini na kusubiri kunyanyaswa na serikali hii,’’ Olianga alisema.
Wafanyikazi takriban elfu 4000 waliosalia katika serikali ya kaunti ndio watakaoathirika na mpango huo.
Kaunti ililazimishwa kukatiza ghafla dili yake na bima ya AAR baada ya mvutano kuzuka kati yao kwa sababu ya malipo.