Watu Watatu wameaga huku wengine tatu pia wakijeruhiwa katika ajali mbili tofauti katika barabara kuu ya Embu-Mwea, Kaunti ya Kirinyaga.
Kulingana na Kamanda wa wa Polisi, Daniel Kitavi katika kituo cha Mwea Magharibi, ajali ya kwanza ilitukia katika daraja la Gwa Kariba karibu na soko la Difthas ambako Lori lilipoteza mwelekeo na kugongana na Pikipiki.
“Mwendeshaji Pikipiki aliaga papo hapo katika eneo la ajali huku mteja wake akiaga baada ya kufikishwa katika hospitali ya Kaunti ya Kimbimbi”alisema kitavi.
Kulingana na Chifu wa Kata ya Mwea Magharibi, ajali ya pili ilitokea katika eneo la Murubara baada ya gari dogo liliokuwa likisafiri kutoka Embu kuenda Ngurubani kupoteza mwelekeo na kugonga Pikipiki iliyokuwa ikitoka soko la Red soil.
Mwendesha Bodaboda alifariki papo hapo huku dereva wa gari Hilo akikimbizwa hospitalini na majeraha mabaya.
“Dereva wa gari alikuwa akijifundisha. Mwelekezi wake ambaye ni mwanadada waliyekuwa naye, alikuwa anamwelekeza kulihepa Trekta liliokuwa linakuja,”aliongeza Kitavi.
Wenyeji wanaokaa katika barabara hiyo wakiongozwa na Susan Wambui, wanataka hatua madhubuti kuchukuliwa ilikupunguza ajali katika eneo hilo.