• Sun. Apr 28th, 2024

Lamu: Serikali yahimizwa Kuekeza Kwa Sanaa Kuinua Utalii

Aug 24, 2023
392 300

Serikali ya kitaifa pamoja na ile ya kaunti ya Lamu zimetakiwa kuekeza kwenye sanaa kama njia ya kuinua utalii wa taifa.

Mkurugenzi wa wakfu wa Waridi na ambae pia ni mkurugenzi wa shirika la Kwetu In Africa linalojihusisha na mambo ya utalii katika kaunti ya Lamu Jennifer Wairimu amesema serikali inapaswa kuwapa wasanii wa mashinani fedha za kuendeleza sanaa na talanta zao.

Soma:Waridi Calls for Peaceful Campaigns as She Promises The Best for Hongwe

Amesema tayari Kwetu In Africa inashirikiana na wasanii wa mashinani katika kutangaza utalii kwani wageni wao hutumbuizwa na wasanii na waigizaji wa mashinani.

“Wageni wanapo book na sisi tunahakikisha kuwa tumewaeleza wanaweza kuwa na Homestay kwa siku moja kati ya zile siku tatu walizobook. Tunafanya vile kupitia vikundi vya vijana na wanawake na hivyo tunaomba serikali iweze kuwashikilia mkono vikundi hivi kwa kua ni baadhi tu ya mbinu za kupata kujiajiri,” alisema Jeniffer.

(4) Facebook(4) Facebook

Kwa upande wake Shaban Athuman maarufu Sheby Medicine ambae ni balozi wa shirika la Kwetu In Africa katika taifa la Tanzania amesema mataifa ya Kenya na Tanzania yanawaze kushirikiana katika kukuza utalii kupitia sanaa na hatimaye kuinua uchumi wa mataifa hayo mawili.

“Hii inaenda kuimarisha kabisaa uhusiano kati ya Tanzania na Kenya kwenye kutilia nguvu swala la utalii. Watalii wakija kenya pia wanaweza kupata nafasi ya kuenda tanzania kwenye kisiwa cha pemba na pia Zanzibar kwa kuwezeshwa na Kwetu Inn Africa,” Alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *