• Thu. Jul 25th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Mtoto Afariki Watu Wengine 7 Mashakani Kwa Kula Nyama ya Kuku

Aug 19, 2021
778 300

Mtoto mwenye umri wa miaka saba katika Kijiji Cha Igumo, Wodi ya Marimati Kaunti ya Tharaka Nithi ameaga huku wenzake Saba na mtu mzima mmoja wakilazwa katika hospitali baada yao kumla kuku aliyekuwa na ugonjwa.

Charity Kaindi anadai kuwa mwanawe aliitwa na Babu yake Jumatatu jioni na akaenda katika nyumba yake alipokula nyama ya kuku kabla ya kurejea kwao.

Baadaye ndipo Kaindi aligundua watoto wa Jirani yake waliokula nyama ile walikuwa wakiugua kwa maumivu ya tumbo pia. Wanawe wengine walipoanza kulalamikia mumivu y tumbo ndipo alipoamua kumpigia simu mumewe amabaye hufanya kazi katika soko la Marimati ndipo watoto hao walipokimbizwa katika hospitali ya Kaunti Marimati.

Baada ya hali Kuwa mbaya ndipo ilipobainika Kuwa watoto nane walikuwa wameila nyama ile kwa Babu huyo alitambulika kwa Kama Karong’o Makembo.

Friday Nyambura mmoja wa Wajukuu wa mzee Makembo ambaye pia amelazwa katika hospitali hiyo ya Marimati alisema Kuwa Babu yake alimletea nyama ya kuku kazini pake ambapo ni karibu na kwake lakini alishindwa kuimaliza nyama ile kutokana na harufu mbaya iliyokuwa nayo.

Nyambura aliongeza kuwa baada ya muda mchache alianza kuhisi maumivu ya tumbo, kulala na povu kumtoka kwenye mdomo alipofikishwa hospitalini.

Kwa Bahati mbaya mtoto mmoja, aliyetambuliwa Kama Linet aliyekuwa amekimbizwa hospitali ya Chuka alipokuwa atibiwe kwa kitengo Cha hali mahututi(ICU).

Mwanaume Makembo amedhibitisha Kuwa kuku huyo alikuwa mgonjwa kabla ya kuchinjwa na tukio hilo halijawahi kutokea hata wakila kuku aliye gonjeka.

Daktari Mwangangi ambaye Ni Afisa wa Matibabu katika hospitali ya Marimati amedhibitisha tukio hilo akisema nyama hiyo ilikuwa na sumu.

Waliolazwa hospitalini wapo katika hali ya kudhibitiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *