Mungano wa waalimu wa chekechea umekuwa ukishtumu KNUT kwa kuingilia ndani kazi yake na kutafuta wafadhili wa program za ECDE bila ushirikiano wao.
Kulingana na KNUT kila muungano uko sokoni na kwamba hawatishwi na muungano wa waalimu hao wa chekechea dhidi ya kushirikiana na waalimu wa ECDE katika programu mbali mbali.
‘‘Tutaendela kushirikiana na waalimu wa ECDE na kwamba hatutishwa kamwe na huyu Otunga kwa sababu kila muungano upo sokoni yeye afanye kazi yake na KNUT kifanye kazi yake..na kwa waalimu wote wa ECDE ambao wanataka kujiunga na KNUT wafanye hivyo na sisi kama chama tutaendelea kutafuta wafadhili kuwasaidia.’’ Alisema.
Lawrence Otunga ambaye ni katibu mkuu wa Kenya Union of Pre Primary Education Teachers KUNOPPET ameshtumu KNUT kuyumbisha muungano huo kwa kutekeleza majukumu ambayo si yake.
‘‘Tunataka kukionya chama cha KNUT kuwa hatutaruhusu wao kuingilia kazi yetu kama chama na pia hawatashurutisha wanachama wetu kushiriki katika program zao.’’Otunga alisema.