Chama cha Naibu rais William Ruto UDA sasa kiko mbioni kupata wafuasi jiji hili la Nairobi na maeneo mengine na imeamrisha usajili wa wanachama haswa vijana.
Kulingana na kiongozi wa vijana katika chama hicho Victor Ayugi usajili huo unaendelea kwa mtandao na hata katika afisi zao huku akirai vijana kujitokeza.
‘‘Usajili unaendelea na tunataka kuhimiza vijana kujitokeza na kujisajili katika chama hiki ,tuna uwazi na ukweli na demokrasia inayotakikana.’’ Ayuko alisema.
Kulingana na Ayugi UDA imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa hakuna kijana anayepigwa kumbo katika mchujo wa chama yaani party nominations.
‘‘Vijana na hata wagombea wote ambao watashiriki kura za mchujo watapata haki zao kwani hatuna yule ambaye chama kimeandalia tiketi…ni wakati wetu kujituma na kuhakikisha kuwa tumehifadhi viti hivyo uchaguzi mkuu,’’ aliongeza.