• Fri. May 3rd, 2024

KNUT Wataka Serikali Kubeba Gharama ya Mtaala wa CBC

Sep 9, 2021
202 300

Chama Cha Waalimu Nchini KNUT Sasa kinataka serikali kumakini na swala la  mtaala mpya Kwa kuongeza raslimali na kusimamia wazazi yale yanayohitajika Ili kuwapa wazazi kazi rahisi mfukoni.

Wazazi wengi wamekuwa wakilalamikia gharama ya CBC wakisema kuwa ni ghali mno.

Naibu katibu mkuu wa KNUT Hesbon Otieno anasema kuwa wazazi wakisaidiwa basi kuufanikisha mtaala huo utakuwa rahisi.

‘‘Mtaala huu si mbaya kile ambacho serikali inafaa kufanya ni kuhakikisha kuwa wanasaidia wazazi kupata zile zinazotakikana kwa sababu ile bajeti ambayo iliwekwa haitoshi lakini kile ambacho hatuwezi kusema sasa hivi ni kwamba tuondoea mtaala huo.’’ Alisema.

Ameongeza kuwa serikali pia inafaa kuhakikisha kuwa waalimu pia wanatapata mafunzo yanayohitajika na hata mshahara mzuri kulingana na kazi ngumu  wanayofanyia mtaala huo wa CBC.

‘‘Waalimu wanafaa kupata mafunzo ya kutosha kwa sababu hivi karibuni kumekuwa tu mafunzo ya masiku na hivyo basi wengi wa waalimu bado hawajakuwa katika viwango hitajika kufankisha mtaala huo.’’ Otieno aliongeza  

Wazazi wamekuwa wakilia sanaa gharama ya CBC wengi wakisema kuwa ni ghali na imekuwa ikiwaumiza mfukoni ukizingatia hali ya uchumi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *