• Fri. May 3rd, 2024

Chama Cha Mawakili LSK Kufika Kotini Kupinga Mtaala Mpya Wa Elimu

Sep 9, 2021
226 300

Rais wa Chama cha mawakili nchini [LSK], Nelson Havi amesema atawasilisha kesi Kortini wiki ijayo kupinga mtaala wa Elimu wa CBC.

Kupitia Mitandao ya Kijamii, Wakili huyoamesema hili ni kutokana na vilio vya Wazazi na Walezi kuwa mtaala huu ni ghali mno.

“Mtaala huu mpaya haupaswi kuwa ghali na ambao hautawafaa watoto wetu mbeleni,” aliandika Havi.
Kulingana na Wakosoaji wa mtaala huu unawahitaji Wazazi na walezi kutumia hela nyigi Zaidi kuliko Mtaala wa 8-4-4 ambao wanakiri ulikuwa nafuu.

Aliyekuwa katibu wa chama cha Walimu nchini Wilson Sossion pia hapo Awali alisema kuwa mtaala huu mpya umekuja ili kukandamiza Mafaanikio ya elimu nchini. Sossion aliukosoa mtaala huo akisema umetekelezwa katika njia zisizofaa kabisa. Sossion alidai kuwa mtaala huu wa 2-6-2-2 haukufuata itifaki zifaazo katika kutekelezwa.

Kulingana na Sossion, mtaala huu unatumika katika kuwamalizia Wazazi pesa kwa kuwa wanatumia hela nyingi kununua vifaa vya wanao kutumia. Pia aliongeza kuwa Walimu wanapitia wakati mgumu katika kuhakikisha mtaala huo unatekelwza ipaswavyo.

Katika siku kadhaa zilizopita, Wazazi na Walezi wamesikika wakilalama kuwa vifaa ambavyo wanahitajika kuwwanunulia wanao ni bei ghali mno.

“Walimu wanatuitisha vitu kila saa. Vitu vingine ni ghali mno. Kwa sasa tumelewa na janga la Korona. Gharama ya Maisha imepanda sana. Hebu serikali iingilie kati itupe suluhu,” alilalama mzazi.

Mtaala huu ulio idhinishwa mwaka 2017 unaonekana kuwa na changamoto nyingi sana katika kutekelezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *