• Sat. Apr 27th, 2024

Vijana Watakiwa Kutumia Teknolojia Kujiimarisha

Sep 2, 2021
284 300

Vijana wametakiwa kujituma zaidi katika maswala ya kuvumbua na kutumia teknolojia vyema ili waweze kujiimarishaa.

Ndio ujumbe muhimu ambao umetolewa na serikali kupitia wizara ya vijana na hata baraza la vijana nchini wakati wa kutuza wale walioibuka washindi katika ushindani wa mwaka huu ulioitwa Fursa vs Economic Recovery Challenge uliohusisha vijana 1300.

Katibu katika wizara ya mawasiliano  na vijana  Charles Sunkuli anasema kuwa wako macho na mradi unaohusisha vijana na tayari wana mipango ya kuzindua vituo vya vijana kwa kila kaunti.

‘‘Tuko kimasomaso na maswala ya vijana na mwaka huu ushindani huu ulishirikisha vijana 1300 na wengi wameweza kukutangamana na kupata mariafa zaidi tunachofanya  sasa kama serikali ni kuunda makao ya vijana kwa kila kaunti kuhakikisha kuwa wanashirikiana kwa karibu na kukuwepo na pahali ambapo wanatumia kama ofisi.’’ Alisema Sunkuli.

Naye afisa mkuu mtendaji wa Baraza la Vijana Roy Sasaka Telewa ametaka vijana kuendelea kujituma huku akirai wadau katika sekta mbali mbali kukumbatia vijana na kuwasaidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *