• Wed. Jun 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wakaazi wa Dandora Wahimizwa Kuchukua Fomu za Basari Shule Zinapoanza

May 14, 2021
387 300

Wakaazi wa wadi Dandora four na Dandora five wametakiwa kujitokeza tarehe 17 mwezi huu ili waweze kuchukua fomu za basari.

Kulingana na Mwakilishi wa Wadi wa Dandora four Francis Otieno, yuko na fomu 700 za basari na kwamba wanalenga wale wasiojiweza.

“Mjitokeze shughuli itakua ya wazi japo fomu 700 hazitatosha ..najaribu kuzungumza serikali ya kaunti kuangazia idadi hii,” Ngesa alisema.

“Lazima uwe na kitambulisho na kadi ya kura ili tuweze kuzuia wale wanaojifanya lakini hawatoki wadi hii.” Aliongeza.
Kila mwakilishi hupewa fomu 700 inayogharimu shilingi milioni 3.5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *