• Mon. May 6th, 2024

Spika Wa County Ya Nairobi Kuandikisha Taarifa EACC

Sep 29, 2021
282 300

Spika wa bunge la Kaunti ya Nairobi, Benson Mutura na Bodi ya Huduma la Jiji wameitwa mbele ya tume ya kupambana na ufisadi EACC.

Hii ni baada yao Kujaribu kuwateua na kupandisha vyeo wafanyikazi 28.

Katika barua hiyo kwa Mutura, anahitajika mbele ya Tume hiyo Ijumaa tarehe Moja Oktoba saa tatu asubuhi.

Hii leo, Tume ya hiyo itakuwa ikimhoji bwana Willis Okello na Dr. Fatuma Affey. Mwakilishi Wodi Mteule Catherine Okoth Pia atahojiwa ijumaa pamoja na mwenye kiti wa Bodi Bwana Charles Thuo.

” Tume ya EACC ina sababu tosha za kudhibitisha kuwa Bodi ya Huduma za jiji la Nairobi itasaidia pakubwa katika uchunguzi unao endelea na ingependa kufanya mahojiani kama ilivyopanga. Tafadhali wajulisheni wanabodi wengine kuhusu hili na wafie katika makao makuu ya Tume ya EACC,” Ilisoma barua hiyo.

Awali, Tume ya EACC ilipokea barua kutoka kwa Mfichuzi aliyefichuwa kuwa Kaunti ya Nairobi ilikuwa inawapandisha vyeo wafanyikazi kiholela na kwa mapendeleo huku ikidaiwa kuwa wengi walikwa wa jamii moja.

Kulingana na barua hiyo ni kuwa Karani wa bunge, addah Anyango alikuwa anawateua watu wa familia yake na baadhi ya viongozi wa bunge hilo.

“Mnamo tarehe kumi na tatu, Karani addah Anyango aliwasilisha majina katika bodi ya Huduma la Jiji akidai kufanya mabadiliko huku akidai kuongeza nafasi nyingine sita,” ilisoma barua hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *