• Sun. May 19th, 2024

Ukweli Wafichuka Kuhusu Kilicho Sababisha Kukatizwa Kwa Mkataba wa FKF na OdiBets

Sep 24, 2021
208 300

Shirikisho la Soka Kenya (FKF) lilitangaza kuwa limetamatisha Mkataba na kampuni ya Kamari ya Odibets ikiishutumu kamputi hiyo kukiuka makubaliano.

Shirikisho hilo katika ujumbe uliotumwa kwa viombo vya habari lilisema kukomeshwa huko kumetekelezwa mara moja.

Shirikisho la Soka Kenya limekatisha mkatabaushirikiano wake na Odibets mara moja kutokana na kampuni hiyo kukiuka makubaliano.

”Shirikisho linaendelea kujitolea kukuza ushirikiano wa kushinda pamoja kwa faida ya mchezo huo na itaendelea kushirikiana kwa moyo wote na washirika wanaoshiriki kujitolea kwetu na maono ya ukuaji wa mchezo nchini Kenya, “FKF ilisema katika taarifa.

Lakini imeibuka kuwa Odibets ilikuwa imejiondoa kwa muda mrefu kwenye mkataba huo na shirikisho ikitaja ukosefu wa uwazi.

Chanzo kilicho karibu sana na kampuni hiyo kilisema imesikitishwa na jinsi shirikisho hilo lilivyoshughulikia ushirikiano wao na kuchagua kujiondoa.

“Tunazungumza juu ya mamilioni ya pesa ambazo tumekabidhi kwa shirikisho kama sehemu ya ushirikiano wetu kukuza mpira wa miguu mashinani, lakini hatuoni chochote kinachotokea mashinani ,” kilisema chanzo hicho. Odibets inatarajiwa kutoa taarifa kesho Ijumaa kulingana na Mkurugenzi Mkuu wake Dedan Mungai. Mkataba huo wa miaka mitatu wa kima cha Sh127 milioni wa Odibets kwa FKF, ulikuwa na lengo la kukuza mpira wa miguu kutoka mashinani. Odibets pia ilikuwa imekubali kuwa “mshirika wa motisha” kwa timu ya kitaifa Harambee Stars.

Chini ya makubaliano haya, kampuni hiyo ingelipa posho na bonasi kwa wachezaji wa Stars kwenye majukumu yao ya kimataifa.

Kukatizwa kwa mkataba wa Odibets kunajiri miezi miwili baada ya FKF kukatizwa mkataba mwengine wa miaka mitano wa Sh1.2 bilioni na kampuni nyingine ya kamari ‘BetKing’ kwa maridhiano kulingana na shirikisho hilo.

FKF imeshuhudia kuondoka kwa washirika wao kwa sababu tofauti tofauti.

Kwanza ilikuwa Supersport ambao walisitisha mpango wao wa utangazaji wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni moja na Ligi Kuu ya Kenya baada ya shirikisho hilo kuingilia usimamizi na uendeshaji mzuri wa ligi hiyo.

Kampuni ya kamari ya Sportpesa ambao walikuwa wadhamini wa ligi pia waliondoa mkataba wao wa miaka 4 wa KsH 450 Milioni na KPL.

Betking ambao waliingia kuchukua nafasi ya Sportpesa kama wadhamini wa taji pia walitoka katika ushirikiano wa miaka mitano wa Ksh 1.2 bilioni hata kabla ya kumalizika kwa mwaka wa kwanza wa ushirikiano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *