• Thu. Jul 25th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

NMS yalaumiwa kwa kuzembea kazini

Jul 21, 2021
274 300

Wakaazi wa eneo la Eastleigh Nairobi wanalalamikia utupaji taka kiholela tabia ambayo imesababisha uchafuzi wa eneo hilo.

Wakaazi wa maeneo ya Third Street, Airbase Second Avenue, First street, 9th street na Garage wanasema kuwa uvundo unaotokana na taka hiyo ni mwingi na wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kupitia taka.

“Tunahofia yakuwa iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa haraka, haswa katika maeneo ya Airbase ambako mitaro ya maji taka haipo, magonjwa kama vile kipindipindu na mengineyo huenda yakazuka,” walisema.
Aidha, walishutumu Idara ya Huduma kwa Jiji la Nairobi (NMS) kwa kutozungumzia swala hili licha ya wao kutoa malalamishi yao.

“Tupo katika kundi Moja na afisa wa Afya wa Kaunti Ndogo ya Kamkunji lakini tulipomtumia picha ya Hali ilivyo, amenyamaza kana kwamba hamna jambo lolote,” waliongeza wakaazi hao.

“Hapo awali, tulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wakiwakamata wale waliokuwa wakitupa taka ovyo, lakini baada ya NMS kuja, kundi hilo lilitokomea,” waliongeza.

Pia katikati mwa Jiji Pana taka nyingi sana katika haswa katika maeneo ya barabara za Kenneth Matiba, Kirinyaga na chochoro za Moi Avenue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *