• Wed. May 8th, 2024

Makarina Akashifu Mrengo wa Kenya Kwanza Kwa Kuwatumia Vijana

Feb 26, 2022
647 300

Kiongozi wa watu wanaoishi na Ulemavu katika Kaunti ya Meru, Michael Makarina ameusifia utendakazi wa Rais Uhuru Kenyatta kwa miaka mitano iliyopita.

Makarina amesema Walemavu, akina mama makanisa  na vijana wamefaidika kutokana na jitihada za Rais Kenyatta za kuhakikisha Maisha ya Wakenya yanaimarika kupitia miundo msingi.

“Kijana wetu ambaye ni DCI Kinoti aliteuliwa na kupewa cheo hicho na Rais Kenyatta na tumefaidika pakubwa. Leo hii, walemavu akina mama na pia makanisa yanafurahia pesa kutoka kwa serikali kuu ya Uhuru ambapo kwa sasa tuna mabarabara,” alisema Makarina.

Aidha amewashutumu vikali viongozi wa Kenya Kwanza kwa kuzunguka eneo hilo ili kutaafuta vijana watakao tumika kusambaza siasa zao mbovu.

READ ALSO: Makarina Warns DP Ruto Against Mount Kenya  Vote Assurance

“Jana walikuwa huku wakiwatafuta vijana watakowasidia kufanya Kampeni. Hakuna chochote cha maana walichowapea. Nawaomba sana vijana wasikubali kutumika,” aliongeza.

Kiongozi huyu amemwakikishia Rais Kenyatta kuwa atazunguka mlima Kenya kupigia Azimio debe.

“Namwambia Rais Kenyatta kuwa kazi yake huku Mashinani mwa kaunti ya Meru inaonekana na sisi tupo imara,” alisema.

Makarina ameahidi kuzunguka katika eneo pana la Mlima Kenya Kuwarai Wananchi kumuunga mkono mpeperushaji Bendera wa Azimio kwa kuwa ndio chaguo la Rais. Aliongeza kuwa Ruto alianza kufanya Kampeni zake Mapema badala ya Kazi na ndicho chanzo kikuu cha kutosikizana na Rais.

Matamshi yake yanakuja siku kadhaa baada ya Rais Kenyatta kuandaa mkutano katika ikulu ya Sagana Kaunti ya Nyeri alipowarai wakaazi wa Mlima Kenya Kumpigia kiongozi wa ODM Raila Odinga Kura kwa kuwa ataendeleza ajenda zake.

READ ALSO: Makarina Says There’s Malice in Judge Mrimas’ Directive to Jail DCI Boss

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *