• Mon. Oct 2nd, 2023

Wakili Makowade Kuwania Uwakilishi wa LSK Nairobi

Feb 28, 2022
636 300

Kinyang’anyiro Cha viti mbali mbali katika chama Cha mawakili Nchini LSK kimepamba moto na Sasa wakili  Gabriel Owade maarufu kama  Ochi  ama Makowade amejitosa uwanjani kuwania uwakilishi wa LSK tawi la Nairobi.

McOwade ni mzaliwa wa mtaa duni Bondeni  Mathare na lengo lake kuu ni kuimarisha sura ya LSK Nairobi na pia kuleta Imani miongoni mwa wakaazi wa Jiji hili haswa wale wanaotoka mitaa duni.

Amesema kuwa iwapo atachaguliwa pia atahakikisha kuwa wale ambao wako katika maisha duni wanapata haki zao mbali na kupambana mauji ya kiholela mitaani.

‘‘Kitu tunataka ni kuwa yule mtu anawakilisha Nairobi awe amegrow huku juu sisi kama Watu wamegrow huku Mpaka Sasa tumekuwa Wakili challenges zetu ni tofauti yule amegrow kwingine tusema kama Kissi na amekam huku na apractice huku,Sisi kama ni Nairobi ni kama ocha so unaingia unafungua law farm unapata kesi kama Thao na unapata ni wale Watu wametoka mtaani lazima utafute njia ya kumsaidia juu mko na attachment na so lazima umsaidie ..lakini unapata Mtu anatoka huko mtaani ananipigia simu Buda nimeshikwa utapata hata kumcharge ni noma..so tunaneed representative anatoka Nairobi mwenye anaelewa challenges kama Hawa wasee…” Owade aliambia kituo kimoja cha habari.

Ametaka wanachama wa LSK kuhakikisha kuwa wanamchagua yule amabye anaelewa magumu ya Nairobi na ambao Wana asilia hapa jijini.

Uchaguzi wa LSK ni tarehe kumi mwezi Machi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *