• Wed. May 8th, 2024

Linda Jamii Yapinga Agizo La Rais Ruto Kotini

Aug 22, 2023
232 300

Vuguvugu la Linda jamii linaloongozwa na msomi Fred Ogola hii Leo limewasilisha kesi mahakamani kupinga agizo la Rais William Ruto kuagiza malipo yote ya huduma za serikali kufanywa kidigitali kupitia mtandao mmoja wa e-citizen ifikapo tarehe thelathini mwezi septemba.

Kwa Mujibu wa profesa Ogola serikali haijahusisha uma kikamilifu na kwa sasa hakuna mikakati ya kujumuisha malipo ya serikali za kaunti na Ile ya kitaifa kwani ni kinyume na malengo ya ugatuzi uku akisema kwamba Rais mwenyewe ndio mwenye usukani wa kipekee wa mtandao uo ivyo basi ni kwa manufaa yake kibinafsi.

Aidha imebainika kwamba takriban biashara mia mbili thelathini na Saba zitafungwa na kupelekea wakenya alfu Saba mia mbili thelathi na Saba kupoteza kazi endapo malipo hayo yatahamishwa na kufanywa kwa njia Moja ya e-citizen.

Mahakama imeamuru mwanasheria mkuu na wizara ya mawasiliano kujibu kwa mda wa wiki Moja uku kesi io ikitarajiwa kutajwa tarehe nne mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *