• Wed. May 8th, 2024

PACJA Yaelezea Hofu ya Africa Kuafikia Malengo ya Kongamano Kuhusu Mabadiliko Ya Tabia Nchi

Aug 22, 2023
249 300

Uku yakisalia majuma mawili pekee Ili kufanyika kwa kongamano la Afrika kuhusu mabadiliko ya tabia nchi litakalo andaliwa jijini Nairobi, wito umetolewa na mashirika yasiyokua ya serikali kwa viongozi watakaohudhuria kuhakikisha kwamba matakwa ya wote walioadhirika kutokana na majanga ya mabadiliko ya tabia nchia yameangaziwa.

Kongamano hilo litaleta pamoja viongozi wa nchi za Afrika wakiongozwa na Rais wa Kenya William Ruto.

Akihutubu katika kikao kilichoandaliwa katika mkahawa mmoja jijini Nairobi, Afisa mkuu mtendaji wa muungano wa Afrika wa haki na mabidiliko ya tabia nchi PACJA Mithika Mwenda, ameelezea wasiwasi wao kama mashirika wakisema kwamba Kuna uwezekano mkubwa kongamano ilo ya Afrika kukosa kuafikia malengo yake endapo maswala muhimu ya haki za kibinadamu na masoko ya kabon hayataanaziwa kikamilifu.

Mwenda ametoa wito kwa Rais Ruto na umoja wa Afrika (AU) kusimama kidete na kuangazia maswala hayo na dhiki ya walioadhirika ikiwa ni pamoja na kutoa kauli Moja kama nchi za Afrika kusurutisha nchi zilizostawi kuhusika katika nchia za kupambana na madiliko ya tabia nchi ikiwa na pamoja na kutoa ufadhili ili kupunguza matukio ya nchi izo yanayopelekea majanga kutokea katika nchi za Afrika.

Haya yanajiri uku mashirika hayo yakihimiza nchi za Afrika kuzungumza kwa sauti Moja na kutoa mwafaka ifikiapo kongamano la cop 28  na kupelekea kubuniwa kwa Sheria za kuzuia na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *