Mwakilishi wadi wa Mountain View Maurice Ochieng’ sasa ametaka wakaazi eneo hilo kutumia kituo Cha afya Cha Kangemi-Gichagi kupata Huduma za afya.
Kulingana na Maurice hospitali hiyo kwa Sasa inahudumia watu 150 kwa siku ikiwemo kuwapima magonjwa mbali na kupeana chanjo.
‘‘Ningependa kuarifu wananchi kufika kituo cha afya cha Kagemi-Gichagi ili waweze kupata matibabu kwa sababu kila kitu kiko shuari na hudumu zinaendelea..ile ripoti ambayo niko nayo tunahudumia watu 150 kwa siku.’’ Maurice alisema.

Maurice anasema kuwa ofisi yake kwa ushirikiano na kitengo cha NMS imeanzisha mikakati ya kuhakikisha kuwa Kuna usambazaji wa maji ya kutosha hospitalini humo.
‘‘Shida ya maji tunataka kuondoa kabisa katika hospitali hiyo na tayari tumewasiliana na pande husika NMS na hata kampuni Kenya Power ili maji iweze kusambazwa kutoka kisima kilichochimbwa hapo hospitalini na hata kwa wakaazi walioko karibu.’’ Aliongeza
Tayari eneo limetengwa kuanzisha huduma za kijifungua kwa akina mama.
‘‘Hii hospitali ni level two na hivi karibuni tutanataka iweze kupeana huduma za kina mama kujifungua na mpango huo pia uko mezani na utafanikishwa hivi karibuni.’’ Maurice alisema.