Kitengo cha Upelelezi wa Jinai, DCI kimetoa habari za kufedheheshwa na ujumbe uliochapishwa na gazeti moja humu nchini unaopania kuiharibia Jina Idara ya Polisi.
“Gazeti hilo ambalo kichwa chake cha habari ilikuwa”NJAA YAUMA POLISI BAADA KAFYU KUISHA” ni fedheha kwa shirika linalotegemewa na wananchi kwa kutoa habari tendeti na za kujenga kuchapisha taarifa zisizokuwa na msingi wala maadili hususan kuiharibia Jina idara ya Polisi,” walisema katika Taarifa.
Idara hiyo imesema kuwa mbali na kuwepo kwa maafisa wachache wa usalama wanaoenda kinyume na maadili ya kazi ya Polisi, hiyo haijatosha kuwa sababu kuipaka matope idara nzima ya usalama.
Idara ya DCI imesema kuwa asilimia kubwa ya maafisa wa usalama wanafanya kazi yao kwa ustadi unaohitajika.
“Itakuwa vyema iwapo mashirika ya kutoa habari yatakuwa makini kutoa taarifa za ukweli na zenye manufaa kwa wananchi na wala sio habari za uchochezi na kupotosha zinazojenga taswira mbaya kati ya maafisa wa usalama na wananchi kwa jumla,” walisema
Aidha wamesema kuwa Idara ya Polisi iko imara na itaendelea kumlinda mwananchi na kutekeleza majukumu yake ipaswavyo kwa mujibu wa sheria.