Mbunge wa Mathira, Mheshimiwa Rigathi Gachagua amekamatwa na Maafisa wa Tume ya Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI).
Rigathi alikamatwa mapema hii Leo, mwendo wa saa kumi na moja asubuhi akiwa nyumbani kwake Nyeri.
Wakili wa Gachagua, Wahome Gikonge ameambia Taarifa News kuwa Maafisa hao ambao walikuwa kumi na tano hawakupeana sababu za kumkamata mteja wake.
Akizungumza na ripota wetu kupitia kwa njia ya simu, Mheshimiwa Rigathi amesema kuwa wapo safarini kuja Nairobi katika Afisi za DCI na hajaambiwa sababu zozote za Kukamatwa kwake.
” Sina uhakika ni kwa nini nimekamatwa. Labda nitajulishwa nitakapofikishwa katika Afisi za DCI Nairobi,” alisema Gachagua.
Mapema mwaka huu, Mwezi wa Januari, Gachagua alifika mahakamani akitaka mahakama izulie Kukamatwa kwake kutoka na madai ya Udanganyifu.
Pia kulingana naye, anadai kuwa kamata kamata zake zinatokana na msimamo wake wa kisiasa wa kumuunga mkono Naibu wa Rais, Dk. William Samoei Ruto.