348 300
Afisa wa Polisi anayefanya kazi katika kituo cha Kacheliba eneo bunge la Pokot Kusini ameshtakiwa katika kituo cha Polisi Lwakhakha baada ya kumpiga mke wake na kifaa kisicho julikana kwenye kichwa.
Afisa huyo kwa jina Isaac Ochome Otwane ambaye hakuwa kazini siku hiyo alikuwa na ubishi na mkewe Linet Sikuku Ndiema mwenye umri wa miaka 43 na ndipo alipompiga kichwani kwa kifaa kisicho julikana na akapoteza fahamu.
Mwanamke huyo alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Cheptais anapoendelea kupata matibabu.
Hali yake japo si nzuri. Aidha mshukiwa alikamatwa na maafisa wa kituo cha lwakhakha na atashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu na kumuumiza mke wake.