• Wed. May 8th, 2024

Wizara Ya Afya Yazindua Sensa Ya Kuhesabu Maeneo Ya Huduma Za Afya

Aug 14, 2023
295 300

Waziri wa afya Susan Nakumicha hii Leo katika makao makuu ya wizara amezindua rasmi zoezi la kuhesabu hospitali na maeneo ya kutoa huduma za afya KOTE nchini litakalofanyika kwa kipindi Cha majuma mawili.

Akiongea katika hafla io waziri Nakumicha amesema kwamba wizara yake inatilia mkazo kuwepo kwa wahudumu wa afya wenye tajriba ya juu na ubora wa bidhaa za afya ili kufanikisha meadi wa serikali wa UHC.

Aidha Nakumicha amesema kwamba wizara yake itashirikiana na serikali za kaunti,mashirika ya kibinafsi na Yale ya kidini Ili kupata idadi kamili ya maeneo yanayotoa huduma za afya Ili kuboresha uekezaji,miundo Maingi,bidhaa za afya na tekinolojia.

Zoezi ili la sensa litafanikishwa na maafisa wa wizara ya afya ,mashirika ya ubora na serikali za kaunti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *