• Sun. May 5th, 2024

Sita Wakamatwa Huku Pombe ya Shilingi 500,000 Ikinaswa

Sep 27, 2021
350 300

Maafisa wa Polisi katika mtaa wa Soweto Kayole jana walinasa Chang’aa ya shilingi Elfu mia tano.

Chang’aa hiyo ilikuwa lita Mia tano thelathini na ilikuwa kwenye mitungi huku nyingine ikiwa imepakiwa kwenye makaratasi.
Kulingana na OCPD wa kaunti ndogo ya Njiru, Paul Wambugu muuzaji wa Chang’aa hiyo amekuwa mafichoni tangia Oparesheni hiyo kuanza.
Wambugu alisema kuwa walifahamishwa kuhusu pombe hiyo haramu na Umma baada ya magari mawili kuleta pombe ile pale na kuenda.
Mwanamke aliyepatikana katika nyumba hiyo ambako pombe hiyo ilinaswa atafikishwa katika mahakama za Makadara na kufunguliwa mashtaka.
Aidha watu wengine watano waliopatikana wakinywa pombe katika nyumba hiyo pia walikamatwa na wanazuiliwa katika kituo Cha polisi Njiru.
Bwana Wambugu amewataka wazazi Kuwa makini na wanao wakati huu kwa Kuwa imeripotiwa wanakunywa pombe haramu kwa wingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *