• Wed. Sep 18th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

‘Nilibakwa na Wanaume 9 Wakaingiza Chupa Sehemu Zangu za Siri’ Mwanamke Aeleza Unyama Uliompata

Aug 5, 2021
867 300

Huku vita dhidi ya dhulma za kijinsia zikiendelea, Winfred Awino msichana mwenye umri wa miaka 23 amejitokeza na kulezea jinisi alivyobakwa na wanamume tisa wasiojulikana waliometaka nyara katika mtaa wa buruburu hapa Nairobi alipoenda kutafuta kibarua.


Kulingana na Awino alitoka nyumbani kwao Utawala kutafuata kazi ya kufua mtaa wa buruburu na ni hapo ndipo akafumaniwa na watu hao waliombaka na kuingiza chupa sehemu zake za siri na kumtupa barabarani.


‘‘Nilikuwa nimesimama mbele ya lango kujaribu kusubiri kazi ya kufua ghafla wanaume takriban tisa wakatokea na nikaskia kitu kimenipiga kichwa upande wa nyuma nikazirai na kuanguka chini..nilijihisi nikiwe eneo fiche kama damu inanitoka baadae wakaingiza vigae vya chupa kwa sehemu zangu za siri.’’ Winfred alifichua.


Alipokea matibabu katika Hospitali ya Mama Lucy ambapo msamaria mwema alimpeleka.


‘‘Chupa hiyo nilitolewa baada ya mwezi mmoja awali sikujua kuna chupa ilibaki ndani lakini baadae nikawa naskia uchungu sehemu zangu nyeti haswa nikitembea.’’ Aliendelea kueleza.


Ameambia Taarifa bNews kuwa kufuatia kubakwa kwake mamake aliaga baada ya kusongwa na mawazo chungu nzima.


‘‘Ilinichukua muda kumweleza mamangu ambaye pia alikua anaugua kuhusu jambo hili, lakini kupitia jama kwa jina Kamau nilifanya hivyo lakini kwa bahati mbaya alisongwa na mawazo na kufariki..’’ aliongeza.


Winfred baadae alishirikishwa katika shirika la Center for Rights Education and Awareness (CREAW) tawi la Kibra ambapo amekuwa akipokea ushauri nasaha.


‘‘Creaw imekuwa ikinisaidia kwa mambo mengi sana,wamenipa fedha kujisadia pamoja na familia yangu,wamenishirikisha kwenye mashirika mengine ambayo pia yamekuwa yakinisadiai sana.’’Winfred alisema.


Mmoja wa watoaji ushauri nasaha katika shirika la Creaw Phoebe Nzulu anasema kuwa wamekuwa wakishirikiana naye kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hajaathirika na msongo wa mawazo.


‘‘Kesi ya Winfred ni ya kutamausha kweli na tumekuwa naye karibu sana kumpa ushauri nasaha na hata kumshirkisha na mashariki mengine ili kupata usaidizi haswa programu za kuinua kinamama kama vile kibiashara.’’ Phoebe alieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *