• Fri. Apr 26th, 2024

MCA Imwatok Ashika Aladwa Tai Kuhusu Ziara ya Sifuna Makadara

Dec 20, 2021
436 300

MCA wa Makongeni Peter Imwatok ametaka mwenyekiti wa chama cha ODM Nairobi George Aladwa kuwa na heshima kwa viongozi wa chama hii ni baada ya Aladwa kukushifu katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna kutokana na ziara yake wikendi wadi ya Makongeni.

Wikendi Sifuna alikua  Makongeni  baada ya kualikwa na mwakilishi wadi Peter Imwatok katika fainali za tonament ya Azimio la Umoja ambayo  ilidhaminiwa na Imwatok na kuhudhuriwa na wanasiasa  kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa.

Kulingana na Imwatok  ameskitika kupata taarifa hiyo huku akisema kuwa mbunge Aladwa alikuwa amealikwa lakini hakuhudhuria.

 ‘‘Tulimwalike Aladwa lakini yeye hakukuja sasa tunashangaa anazunguka kwa mtandao akishtumu katibu wetu Edwin Sifuna …lazima Aladwa aambiwe si lazima kiongozi wa chama cha ODM akija sehemu fulani yeye lazima aarifiwe huyu ni kiongozi wa chama cha kitaifa si ya makadara pekee..Tuwe na heshima na lazima tutapamna naye rasmi chamani.’’Imwatok alisema.

‘‘Ju Nairobi sio yako na  kila kiongozi wa chama hiki cha ODM yuko huru kutembea popote kwani wewe ndio nani jameni…tulikualika ukadinda kufika kwani ilikua tukulazimishe.’’ Imwatok  aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *