• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Mashirika Ya Serikali Sharti Yawajibike Asema Mbunge Kirwa

Jan 26, 2023
401 300

Mbunge wa eneo bunge la mosop Abraham kirwa ametoa wito wa kufanyiwa mabadiliko na kubinafsishwa kwa sekta za serikali ambazo miaka nenda miaka rudi zimekua zikirekodi hasara kwa mauzo kama shirika la ndege la Kenya airways,baadhi ya hoteli za kifahari kama safari lodge ambayo licha ya kua karibu na hoteli maarufu ya pride inn ambayo inanogesha biashara safari lodge kwa kinaya imekua ikirekodi hasara Kila mwaka,izi ni miongoni mwa biashara zingine ambazo zimetiwa kwenye darubini kwa usimamizi mbaya

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa katika kongamano la wabunge linaloendelea mbunge uyo amesema kwamba ni sharti kwa mashirika yote serikali kuhakikisha kwamba yamewajibika na kufanya kazi kama inavyostahili na kurekodi faida ili kuendeleza miradi yote ya serikali.

Kwa mujibu wa mbunge wa Mosop,serikali imekua ikipoteza kiwango kikubwa Cha hela kupitia kuekeza kwa mashirika ambayo yanafifia kutokana na ufisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *