345 300
Mwanamke mwenye umri wa Miaka 27, mama wa watoto watatu katika Kaunti ya Machakos alifikishwa mahakamani hapo Jana baada ya kumua mwanawe mmoja kwa sumu huku mmoja akiponea baada ya kukimbizwa hospitalini.
Mary Nduku anadaiwa kufanya kitendo hicho baada ya wazazi wake kumkanya kukatiza uhusiano wa kimapenzi na Mjomba wake.
Mary anadaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mjomba wake mwenye umri wa Miaka 27 na baada ya Mamake Teresia Mwikya kumkanya, ndipo alipojaribu kuwaua wanawe wawili siku ya Jumamosi.
Watoto hao walikimbizwa hospitali ya Machakos lakini yule mdogo akaaga alipofikishwa hospitalini. Mwenzake bado amelazwa na anapokea matibabu.
Kesi hiyo itatajwa mnamo Agosti 2.