400 300
Watu Watatu walifikishwa kwenye Mahakama za Kibera baada yao kupatikana na Nyama kilo 1500 ya Punda Milia.
Watatu hao, Onesmus Thyaka Munyao, Sammie Oyaro na Francis Kimani Walishtakiwa kwa kukiuka Sheria za Wanyamapori za Mwaka 2013 kwa kupatikana na Nyama ya Wanyama wa mwitu bila idhini ya Maafisa wa Mbuga (KWS)
Watatu hao wanadaiwa kupatikana wakipima nyama kilo mia mbili walipopatikana na maafisa wa Polisi wa kituo Cha Shauri Moyo.
Walikuwa pia wameweka kilo mia nane kwenye ndoo na Majokofu.
Watatu hao walikana mashtaka hayo wakiomba kuachiliwa kwa dhamana, huku wakijitetea kuwa ni waajiri wa kawaida tu na familia zao zinawategemea.
Si mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea.