• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Kampeni za Chama cha Wahadhiri UASU Zimepamba Moto Uchaguzi Ukinukia

May 22, 2021
941 300

Huku uchaguzi wa chama cha wahadhiri nchini UASU ukiendelea kukaribia wagombea wameebdelea kuuza Sera zao katika matawi ya vyuo vikuu mbali mbali.

Kundi linaongozwa na katibu wa sasa Constantine Wasonga limekuwa Pwani kushawishi wahadhiri kuwapigia kura kwa awamu nyingine ya miaka mitano.

Onesmus Mutio wa kundi hilo anasema kuwa nia yao kuhakikisha kuwa maisha ya wahadhiri yamebadilika na ajenda yao ya kwanza kuhakisha utekelezwaji wa CBA zote zilizopigwa sahihi.

“Tumekuwa Pwani tukitafuta kura chini ya kundi la Wasonga Fresh nia yetu ni kuhakikisha zile CBA zote zilizowekwa sahihi ikiwemo ile ya 2017-2021 imefanikishwa kikamilifu,” alisema.

Wasonga anatetea kiti chake cha  katibu mkuu huku  Muga Kolale akitetea kiti chake cha uenyekiti.

Onesmus Mutia anataka kiti cha mratibu mkuu wa chama.

Uchaguzi huo utafanyika tarehe 23 Juni mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *