Hospitali ya Gichagi-Kangemi Mountain View imekamilika na sasa kitengo cha Nairobi Metropolitan Services,Wakilishi na wadau wengine wanafanya matayarisho ya ufunguzi wa kituo hicho cha afya.
Mwakilishi wadi wa eneo hilo Maurice Ochieng’ anasema kuwa ni hospitali ya kwanza katika eneo hilo tangu Kenya ijinyakulie uhuru na hivyo basi itawasadia wakaazi zaidi kwa maswala ya matibabu kwani huwa inabidi watafute matibabu Kangemi Health Centre ambapo ni mbali.
Maurice alisema ‘‘Ni mwamko mpya kwa wakaazi wa Mountain View na tunataka kushukuru wadau wote sana sana NMS kwa kutuletea hospitali, nimepambana sana kuhakikisha kuwa imejengwa hapa kwa manufaa ya watu wetu.’’
Kina mama pia wataweza kujifungua katika hopsitali hiyo.
‘‘Ni level two na hii ina maana kuwa kina mama wetu wataweza kujifungua papa hapa bila kujisumbua kwenda hospitali za mbali,’’aliongeza