• Sun. May 28th, 2023

Kamati ya Ukaguzi wa Fedha yawaonya maafisa wa Kaunti kutosusia mikutano yao

Feb 22, 2023
120 300

Wawakilishi wodi wa Kamati ya Ukaguzi wa Matumizi ya Fedha katika bunge la Nairobi wametishia kuwachukulia hatua maafisa wa Kaunti ya Nairobi watakao kosa kufika mble ya Kamati hiyo na kuwasilisha ripoti kulingana na uchunguzi wanaondeleza kubaini matumozi ya hela kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa fedha za Umma Nancy Gathungu.

Wakiongozwa na Nwenyekiti wa Kamati hiyo na Mwakilishi wodi wa Ngara Chege Mwaura, Wawakili hao wamewapa Maafisa hao wa Kaunti siku kumi na nne ilikuwasilisha ripoti yao mbele ya Kamati hiyo.

“Tunaelewa tu kwa sasa kwa Kua walipeana taarifa za kutofika leo mapema ndio maana tumeamua kuwapa siku kumi nanne. Tunatarajhia watakua wametimiza jukumu lao,” Chege alisema.

Kamati ya Ukaguzi wa Fedha Kaunti ya Nairobi katika kikao chao cha Februari/22/2023. Picha/Hisani

Kamati hii inamuda wa hadi kabla ya kutamatika kwa mwaka huu wa kifedha kupeana ripoti yao ya uchunguzi wa ripoti tisa zilizotolewa na Mkaguzi wa matumizi ya pesa za Ummma.

Pia, Kamati hii ina tarajiwa kuendeleza vikao vyao na maafisa zaidi kabla ya kuandika ripoti za mwisho.

“Tunatumai kabla ya kutamatika kwa mwaka huu wa kifedha, tutakua tumemaliza vikao vyetu na kupeana ripoti,” Mwaura aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *