• Thu. Jul 25th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Imwatok Ndiye Kiranja Upande Wa Wachache Spika Mutura Asema

May 26, 2021
283 300

Spika Wa bunge la kaunti ya Nairobi  Ben Mutura ametupilia mbali jaribio la mageuzi ya uongozi wa wachache ambapo Peter Imwatok anadaiwa kuondolewa kama Kiranja wa wachache .

Kulingana na barua kutoka kwa Mutura bwana Imwatok ndiye kiranja  halisi upande wa wachache na kwamba jaribio la kumtoa lilifanywa  kinyume na sheria za bunge.

‘‘Hii ni kudhibitisha kuwa nilipata barua kutoka kwa chama cha ODM kikisema kuwa kuwa hakijafanya mabadiliko yoyote katika uongozi wake katika bunge hilo na kwamba pia nakubuliana na naibu kiranja wa wachache Moses Ogeto kuwa sheria haikufuatwa kumwondoa Imwatok,’’ Mutura alisema.

Hayo yakijiri chama cha ODM  kupitia katibu wake Edwin Sifuna kimeweka wazi kuwa watafanya mkutano leo na kuwapa barua wakilishi wadi kaunti ya Nairobi waliohusika katika jaribio hilo kwani hata baada ya kukomeshwa na chama hawakutii.

 Sifuna alisema, ‘‘tumechoka na sarakasi za wakilishi wa chama na ni nkweli tutafanya mkutana na kuwapa barua za kinidhamu.’’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *