Watu zaidi ya kumi bado hawajulikani waliko kufuatia mkasa wa moto ambapo lori liliokuwa limebeba mafuta ya petroli kulipuka na kuwacha watu 13, wakiwa wamefariki na wengine 31 wakijeruhiwa kule kijiji cha Malanga Gem kaunti ya Siaya.
Ajali hiyo ilikuwa imehussisha lori ya petrol liligongana uso kwa uso na lori ya maziwa katika barabara ya Busia –Kisumu na wakaazi wakalivamia na kuanza kuchota mafuta.
Kamanda wa polisi eneo la Gem Charles Chacha amedhibitisha kuwa watu 13 wamefariki huku wengine 24 wakilazwa.
‘‘Kwa sasa tunaweza fifo vya watu kumi na tatu lakini tunashirikiana ili kujua ikiwa wengine waliangamia zaidi na kutotambulika.’’ Chacha alisema.
Kufikia sasa bado walioteweka wanatafutwa huku wakaazi wakisema kuwa huenda wengi wamefariki.
Tom Omondi anasema kuwa ndugu yake alienda kuteka mafuta katika eneo la mkasa lakni mpaka sasa hivi hajaonekana.
‘‘Alichukua kibuyu na kukimbia kuleta mafuta na kwa harakati hizo mpaka sasa hivi hatujamwona hatujui yuko wapi lakini tunahofu mkubwa huenda aliangamia,’’ Tom aliambia Taarifa News.