• Wed. Jun 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Babake Mshukiwa wa Mauaji ya Polisi Aweka mambo Bayana

Jul 19, 2021
321 300

Babake Mshukiwa wa Mauaji ya Afisa wa Polisi kule Nakuru na Mfanyibiashara Kule Kule, Caroline Kangogo amepuuzilia mbali madai kuwa mwanawe aliuawa.


Familia imesema kuwa atazikwa tarehe 24 kwao Iten na hatachomwa kama vile Ombi lake lilivyokuwa.


“Sitaka uvumi ya watu kusema pengine aliuawa. Yule mtu anajua aliuwawa anaweza kujitokeza na atueleze, sababu ile kitu mimi niliona ni huyu msichana

mwenyewe alijiua kulingana na vile tulimpata,” alisema.
Kulingana na Mzee Kibor, mwanawe aliletwa saa Nne Usiku hii na Bodaboda ambaye hata hakujuwa kuwa aliyekuwa amembeba alikuwa Kangogo.


“Huyo kijana hakujua huyo ni msichana wangu, alimleta tu kama abiria yeyote akakuja akamwacha hapa barabarani karibu Mita 50 kutoka nyumbani,” aliongeza.


Aidha aliongeza kuwa ni uchungu kwao kama familia kwa kuwa kila mtu anasema kile anachiktaka kumuhusu mwanao.


“Risasi vile ilitoka haingesplash kwa ukuta kwa sababu kulingana na risasi mahali ilitokea ilitokea upande wa mdomo chini na ikatokea karibu upande wa kushoto ya kichwa yake …alipiga kutoka upande wa kulia na ni kama alipiga ikielekeshwa ni kama juu kidogo……..so haikusplash kwa sababu risasi ingetokea upande wa mbele kutokea nyuma…Caroline ni mtu wa kulia si mtu wa kutumia kushoto, kuandika kufanya kazi yake yote anatumia kulia,” alisema Kibor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *