• Fri. Jan 27th, 2023

Wanahabari wahimizwa kuhubiri Amani kabla na Baada ya Uchaguzi

Aug 3, 2022
119 300

Wanahabari wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri amani zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Uchaguzi.

Kulingana Shirika lisilo la Kiserikali la Eminent, hii itasaidia katika kudumisha Amani kabla na baada ya Uchaguzi.

Baadhi ya vitu ambavyo wametakiwa kuilia maanani ni; Kupeana habari zilizo dhibitishwa na haziwagawanyi wakenya wala kuwatia wasiwasi na uwoga.

“Wanahabari ndio nguzo kuu Katika Kuhubiri Amani. Wacha tuhakikishe kuwa tunapeana habari zilizo dhibitishwa na za kweli. Tusiwatie wakenya uwoga kwa kupeana habari nyingine zilivyo,” alisema Mwenye kiti wa Eminent.

Aidha, wametakiwa kuwakemea wale wanaoendeleza vurugu bila ya kuegemea upande wowote huku wakiambiwa kuwa wanafaa kufikiri maisha baada ya sias.

Pia wanasiasa wamehimizwa kutumia lugha safi katika kampeni zao bila ya kuwagawanya wakenya kwa matusi.

Wanahabari wametakiwa kuzingatia Usalama wao mwanzo kabla ya kuripoti habari zozote.

“Wanahabari ni kiungo muhimu katika kueneza habari. Hawafai kuegemea upande wowote. Wacha tupeane habari sahihi kwa wananchi na kuwapa matumaini ya kuwa pana maisha baada ya sias,” aliongeza.

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya Uchaguzi, Wanahabari wameahidi kutilia maanani haya yote ili kutimiza malengo sawa na yale ya tume ya uchaguzi na Mipaka (IEBC)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *