• Sun. Jun 23rd, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wanachama wa UDA Walalamikia Wizi wa Kura Kiambaa

Jul 15, 2021
234 300

Mwanaiji wa chama Cha UDA John Wanjiku amepinga vikali hatua ya baadhi ya wabunge wa Jubilee kuingia katika vituo vya kupiga kura.

Kulingana na Wanjiku kulikua na makubaliano baina ya IEBC na wabunge kuwa viongozi hao hawatakubaliwa kupiga Kambi katika vituo vya kupiga kura.


“Tunakashifi visa vya kuhongwa kwa wapiga kura na pia hakuna mbunge anafaa kuruhusiwa kuingia kitu tunashanga kuona wengine wakiruhusiwa,” Wanjiku alisema.


Haya yakijiri mbunge wa Maathira Rigathi Gachagua amedai kuwa Kuna visa vya Wizi wa kura haswa kwa kutumia machifu madai ambayo yamepingwa na maafisa wa IEBC kituo Cha kupiga kura Thimbigua.


“Kuna wabunge wa Jubilee ambao wanaingia vituoni kinyume na jinsi tulivyoagana si sawa… machifu wanatumiwa pia kuhonga wapiga kura tunataka kuwaambia wakome,” Gachagua alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *