• Wed. Dec 11th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Uchunguzi kati ya Uhusiano wa Malaria na Virusi vya Corona kutolewa mwaka ujao

Jun 1, 2021
483 300

Maafisa wa Uchunguzi katika Taasisi ya Matibabu na Utafiti (KEMRI) walianzisha uchunguzi wa Miezi kumi na nane mnamo Januari ili kubaini jinsi ya kushughulikia virusi vya Korona kwa mgonjwa aliye na Malaria katika maeneo ya Nyanza na Magharibi ambayo huathirika na gonjwa la Malaria.

Katika majuma kadhaa yaliyopita, pamekuwa na Ongezeko la idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona katika Kaunti za eneo la Nyanza.

Katika taarifa kwa wanahabari hiyo Jana, Dr. Hellen Barsosio, alisema kuwa wale walio na magonjwa ya Sukari na Msukumo wa Damu ndio walio dhaniwa kuathirika na Virusi vya Korona, lakini pia uchunguzi unafaa kufanyiwa ili kubaini ni vipi wale walio na Malaria wanavyopaswa kutibiwa Virusi vya Korona.

“Wakati janga la Korona lilipoanza tulisema kuwa wale walio na magonjwa ya Sukari na Msukumo wa Damu ndio wanaoathirika zaidi. Lakini, wale ambao wanapatwa na Malaria pia wapo katika hatari na tunafaa kujua ni vipi wanapaswa kushughulikiwa,”alisema Dr. Hellen.

Uchunguzi huu unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka ujao. Hili litaweza kusaidia kujua ni vipi wanaoishi katika eneo Pana la Magharibi na Nyanza ambao hukumbwa na Malaria watakavyoshughulikiwa wanapoambukizwa virusi vya Korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *