576 300
Waumini dini ya Kiislamu katika mtaa duni wa Korogocho wamepata mapochopocho kusheherekea Eid hata wanapomaliza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Kampuni ya SecurKenya Limited kwa ushirikiano na mashirika ya jamii yamepeana vyakula waumini hao ili waweze kupata wanachoweza kutia tumboni wakati huu wa Eid.
Benjamin Mossas anasema “sisi kama kampuni si Mara ya kwanza kufanya hivi ..tuwe na moyo wa kutoa kwa wasiojiweza nasi pia tubarikiwe.”
“Tumepata chakula Mungu abariki wahisani na ni kweli hatukuwa na lolote kusheherekea EID,” Salama Ali alisema.
Kilele za sherehe za Eid ni leo jioni mpaka hapo kesho.