• Sun. May 19th, 2024

Raila Aahidi Kuongeza Soko La Miraa Kongo na Somalia

Oct 18, 2021
381 300

Kinara wa ODM Raila Odinga amewaahidi wakulima wa miraa Meru that he kuongeza soko la Miraa iwapo atachaguliwa kuingia ikulu mwaka ujao.


Odinga ameongea alipokuwa mji Mau kaunti ya Meru hii leo Raila yuko ziarani sehemu ya mashariki ya mlima Kenya kwa siku tatu.raila ameahidi kuimarisha biashara ya miraa katika nchi za Congo (DRC) na Somalia.
Pia ameahidi kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Kenya na Somalia iwapo ataingia Ikulu.


“Mimi najua wakulima wa miraa wamepata shida mingi kwa kukosa soko…ile soko yetu ya Somalia inadidimia, mara wamefunga mara wamefungua…Ntahakikisha ya kwamba Somalia inafungua mipaka yake na miraa inaenda huko,” alisema.


“Kuna sehemu ya Somalia ambayo imekuwa huru, inaitwa Somaliland, tayari wamekubali kuchukua miraa kwetu, lakini Somalia imezuia ndege yetu kupita na kupeleka miraa huko. Tutatatua shida hilo, ndege yetu itoke hapa ifike kule Somaliland.”


“Mimi ni rafiki sana ya rais wa DRC Tshisekedi, nitaongea nay eye akubali miraa ytu iingie kwa soko ya DRC…na vilevile majirani wetu hapa chini. Vilevile tutaendelea kuzungumza na serikali ya ulaya maanake hakuna thibitisho eti miraa inaathiri maisha ya watu,”aliongeza.


Raila pia ameutetea mpango wake wa kupeana shilingi 6000 kwa kila familia. Amewakashifu wapinzani wake wanaolalama kuwa matumizi ya serikali yatakuwa yameongezeka hadi Ksh.150M.


Raila ameaahidi kuziba nyufa zote za ufisadi na kuhakikishsa hela hizo zinatumika Kufanya miradi ya maendeleo. Ametoa madai kuwa Kenya hupoteza Shilingi Milioni mia sita kila mwaka kwa Ufisadi.

READ ALSO:‘Nilibakwa na Wanaume 9 Wakaingiza Chupa Sehemu Zangu za Siri’ Mwanamke Aeleza Unyama Uliompata


“Tutapigana na ufisadi…ufisadi ndio adui mkubwa ya Wakenya…saa ile mtu anaingia pale yeye ni mwembamba kama sindano, baada ya mwaka mmoja (amenona),” alisema Raila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *