• Sun. May 19th, 2024

Mashirika Ya Kijamii Yaapa Kupambana na Serikali Katika Mahakama Ya Rufaa

Oct 18, 2021
339 300

Mashirika ya kijamii yakiongozwa na Katiba Institute ,Kenya Human Rights Commission,Nubians Right Forum na mashirika mengine sasa yanasema kuwa yako tayari kupambana na serikali katika mahakama ya rufaa kuhusu uamuzi uliopigwa breki upeanaji wa Huduma Namba.

Robert Waweru kutoka shirika la Kenya Human Rights Commission, anasema kuwa wamejitayarisha vilivyo kuhakikisha kuwa serikali imehesheshimu haki za wakenya kabla ya upeanaji wa kadi zaa Huduma Namba.

Hayo yametiwa manani na mwenyekitiwa  wa Nubians Right Forum Shaffi Ali ambaye kwanza amepongeza mahakama kuu kwa kuhakiksiha kuwa sheria inafwatwa.

Kulinganan na Shaffi wao kama Jamaii ya Wanubi walikuwa wametengwa kabisa katika zoezi la upeanaji wa  Huduma Namba kwani wengi katika jamii hiyo hawana vitambulisho.

READ ALSO:Washukiwa 2 Wa Mauaji Wakamatwa

“Leo tumetoa hiyo press statement kushukuru ile hukumu iliyopelekwa na wenzetu kutoka Katiba institute. Hukumu iliyotolewa kuhusu uhakiki wa data.Tuanambia serikalii kuwa kila kitu hufuata sheria. Dr. Matiang’i na Kibicho wajue afisi zile ni za wakenya. Lazima watafanya vitu kulingana na sheria na kuhakikisha usawa,” alisema Shaffi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *