Maafisa katika kituo Cha Ruai, Kaunti Ndogo ya Njiru wanaendeleza uchunguzi baada ya Jamaa mmoja kuuawa katika kisa Cha kutatanisha.
Mwanaume huyo, John wambugu Waithera aliuawa na Kundi la watu walio mdhania kuwa mwizi.
John ambaye alipata ajali miezi kadhaa iliyopita na kupoteza Kumbukumbu zake, alikuwa amepona na akaamua kurejelea tabia yake ya ulevi alipokumbana na mauti yake.
Siku hiyo alipouawa, inadaiwa kuwa John alienda kunywa pombe kilomita tatu kutoka kwake na akapoteza kumbukizi zake. Ilipofika saa Moja, alikuwa amepata ufahamu kiasi na akaanza kurejea nyumbani kwake, ambako ni Karibu na kituo Cha Polisi Cha Ruai.
John alienda kwa jirani zake na alipokuwa akikaribia kufungua mlango, umati wa watu ulijitokeza na kumpiga kitutu wakimshitumu kuwa mwizi.
Wakaazi hao walisema kuwa katika siku za karibuni, wamekuwa wakiibiwa Sana ndiposa wakaamua kuchukua Sheria mikononi mwao.
Baada ya kugundua amefariki, waliutupa mwili wake mita mia mbili kutoka eneo alipopatikana na jamaa zake.
Wakizungumza na Taarifa News, rafiki zake wamemtaja kuwa alikuwa sio mwizi na alikuwa tu amepoteza fahamu.
“John hakuwa mwizi, alipoteza tu fahamu,” walisema.
Familia yake ikiongozwa na kakake, Michael Maina inataka atendewe haki.
Polisi kwa sasa wanawazuilia washukiwa wawili huku wakiendeleza uchunguzi.