• Mon. Oct 7th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Polisi Kumaliza Kundi Haramu la Apana Tambua Dandora

Jul 5, 2021
490 300

Polisi sasa wametoa onyo kali kwa wale wahalifu wa kundi haramu linalojulikana kama Apana Tambua Polisi ambalo tena limechipuka katika maeno ya Dandora na linahangaisha wananchi.

Kulingana na kamanda wa polisi katika eneo hilo Adamson Bungei hawatarushusu hilo tena na watapambana vilivyo na wahalifu wanaohusika.

‘‘Nataka kuweka wazi kwamba tutapambana na kundi hili mpaka pale litazima kabisa na kwa vijana wetu hakuna ushindi katika uhalifu,’’ alisema.

Wikendi mhalifu kutoka kundi hilo alipigwa risasi na poilisi hadi kufa baada ya kumnyanganya James Onyango shilingi elfu 10,  simu mbili .

Wengine wane walitoroka huku msako dhidi yao ukiendelea.

‘‘Huyu ambaye aliangamia mkononi mwa polisi wikendi amekuwa mhalifu sugu na miaka mitatu iliopita alikua gerezani.’’ Bungei aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *