• Fri. May 24th, 2024

Mwanaume Ashtakiwa Kibera Kwa kumdhulumu Mwanawe wa Kambo.

Jun 9, 2021
454 300

Mwanaume wa umri wa Makamu katika eneo la Kibera ameshtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mwanawe wa kambo wa miaka minne.


Mwanaume hyo kwa jina Patrick amesemekana kumdhulumu mtoto huyo mara kadhaa nyumbani kwake wakati ambapo mamake hayupo nyumbani. Patrick alishtakiwa katika mahakama za kibra na kupelekwa katika gereza la maeneo ya viwanda huku uchunguzi ukiendelea.


Kulingana na ofisa wa watoto katika eneo la kibera Humphrey Lando, ni majirani ambao wamekuwa wakiyaona madhila hayo ambao waliwataarifu maafisa wa Polisi ambao walimkamata kwake pale Mwembeni.
“Tulimpata mtoto akiwa kwnye sakafu na vidonda ishara tosha kuwa alidhulumiwa,” alisema Lando.


Aidha, mtoto huyo ambaye anashughulikiwa na serikali kwa sasa alitibiwa katika hospitali ya DC Kibera.


“Tunawasidia Polisi katika kuukamilisha uchunguzi, lakini Koti iliamuru tusalie na mtoto mpaka kesi itakapokamilika,” Aliongeza.


Katika siku za hivi karibuni pamekuwa visa vingi vya Wazazi kuwadhulumu na hata kuwanyanyasa kimapenzi wanawao wa Kambo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *