Wakaazi katika eneo la Kakamega wamejitokeza na Kulaani kitendo ambapo nyoka alikuwa anasafirishwa katika matatu moja, kisha kutoka na kukanyagwa na matatu nyingine.
Dereva wa matatu alisema kuwa alikuwa katika shughuli za kawaida za biashara ya kuwasafirisha wateja ambako wasafiri waliokuwa wameabiri gari hilo walianza kupiga mayowe asimamishe gari.
Inasemekana, waliokuwa ndani ya gari hilo walimwona nyoka akitoa kichwa ndani ya ndoo iliyokuwa kwenye gari hilo kisha wakaanza kupiga kelele.
Gari liliposimama nyoka alitambaa na kutoka ndani ya gari na kuanza kuenda. Matatu iliyokuwa ikipita ilimkanyaga na kumuua. Dereva wa gari hilo alipotaka kujuwa aliyekuwa na nyoka yule, abiria wote walikana na wakaendelea na safari.
“Tumeshangaa sana na kitendo hiki. Najua yule aliye kuwa na nyoka huyu, atafanya sherehe ya matanga na wanawe kwa ajili mmoja wao ameaga. Kwa mila lazima wafanye sherehe ili liyekuwa na nyoka huyo arudi saw aka sababu najua hatakuwa na Amani na uchangamfu,” alisema mzee mmoja.
“Hata mimi nimelani kitendo hiki sana kwa sababu imetuharibia biashara. Watu wataogopa kupanda matatu kwa sababu watafikiri matatu zote za Kakamega zina Nyoka,” aliongeza dereva mmoja.