• Mon. Apr 29th, 2024

Mfanyakazi auwawa na mbwa wa muajiri wake

Jan 25, 2022
510 300

Mfanyakazi mmoja wa kike wa umri wa miaka 39 katika eneo la Moriema mjini Malindi ameuwawa kwa kuumwa na mbwa wa muajiri wake .

Rosdelyn Nafula alishambuliwa na mbwa huyo katika boma la muajiri wake , baada ya kufungua mahali anakofungwa mbwa huyo wa asili ya Afrika kusini.

Mfanyakzi mwenza wa kiume kwa jina John Siria alisema kuwa aliskia kilio cha mfanyakazi mwenza alipokuwa akishambuliwa na mbwa huyo .

Alikimbia eneo la mkasa na kumuokoa lakini muathiriwa akasema yuko sawa na kwamba atarejea nyumbani mwenyewe kabla ya kupatikana asubuhi akiwa ameaga dunia.

Uchunguzi uliofanywa hata hivyo umebaini kua alikuwa na majeraha mabaya mwilini mwake yaliosababishwa na kung’atwa na mbwa huyo .

Maiti yake imehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya star, uchunguzi ukiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *