• Wed. May 1st, 2024

Mwendwa Ndiye Aliyeteua Kikosi Cha Stars Kilicholishwa Bao Tano-Tetesi

Oct 10, 2021
497 300

Tetesi zimeibuka na kufafanua Ni Nani Aliyekitaja Kikosi cha Harambee Stars ambacho Kililimwa na Mali.


Kenya Harambee Stars ilibomolewa 5-0 na Mali jambo ambalo liliwaacha mashabiki wengi wa Kenya wakifadhaika.

Hii ilitokea chini ya kocha mpya Engin Ferat ambaye alichukua nafasi ya Ghost Mulee aliyejiuzulu. Walakini, habari zinazojitokeza zinafunua kwamba Kocha Ferat hakuchukua jukumu lolote katika kuchagua kikosi bali kazi hiyo ilifanywa na Rais wa FKF Nick Mwendwa.

Kulingana na uchunguzi ulofanywa na Taarifa News, Nick Mwendwa mwenyewe alitaja kikosi cha 11 wa kwanza cha Harambee Stars, huku ikiwa kati ya wachezaji 11, sita walitoka kwa timu ambayo anaimiliki, ambayo ni Kariobangi Sharks.


“Tunaihisi haikuwa Kenya Harambee Stars iliyokuwa ikicheza dhidi ya miamba hao wa Afrika Magharibi bali ilikuwa ni Kariabangi.”

Haya yanajiri huku kukiwa na mizozo ndani ya shirikisho hilo huku idadi fulani ikihisi kwamba shida za mpira wa miguu za Kenya zinapaswa kulaumiwa shirikisho hilo na Nick Mwendwa. Ingawa kocha aliomba msamaha kwa wakenya kwa kichapo hicho.


Aidha tunahisi kuwa Kocha Ferat hakuwa na la kufanya kwani hakupewa nafasi ya kuchagua kikosi kizuri.

READ ALSO:Harambee Stars See Blackout In World Cup Qualifier Match

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *