• Fri. Apr 26th, 2024

Walemavu Mombasa Wahamasishwa  Kuhusu Haki Zao

Nov 18, 2021
387 300

Wale wanaoishi na ulemavu katika maeneo ya Pwani wameendelea kupata ugumu wa kupata  kutambua haki zao na hata huduma za kisheria.

Hii ni kulingana na Wakili Shadrack Wambui wa shirika la Sheria Mtaani  ambaye amekua  Mombasa  kwa ushirikiano na Baraza la Walemavu Nchini

Kulingana na Wambui  taasisi husika bado haijawafikia jinsi invyotakikana kwa walemavu hao, ili kuwatambua na changamoto zinazonazowakumba .

Hii leo shirika hilo la Sheria Mtaani na maafisa kutoka baraza la walemavu nchini wametembea mitaa duni mbali mbali kaunti ya Mombasa  ikiwemo Bombululu,Likoni  katika nyumba  wanakoishi walemavu ili  kuwahamasisha kuhusu haki zao.

‘‘Tumeweza kuzungumza nao kuna usaidizi ambao tumepeana kama vile ushauri nasaha  na  hili si mwisho tutaendelea kushirikiana na baraza hili kuhakikisha kuwa tumefanya Zaidi…hii leo tumezuru sehemu mbali mbali ikiwemo Bombululu,Likoni ambapo tumezungumza na walemavu katika makaazi yao.’’ Wambui amesema.

Shughuli hiyo iling’oa nanga hapo juzi katika uwanja  wa Tononoka na imetamatika leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *